Saturday, September 10, 2011

AJALI YA MELI YA SPISE ZANZIBAR: MATUKIO KATIKA PICHA

NI KIKAO ALICHO KITAYARISHA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE BALOZI SEIF ALI IDDI KWA VIONGOZI WA SERIKALI WALIOKUWEPO KISIWANI PEMBA CHENYE LENGO LA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UPOKEAJI WA WAHANGA WA AJALI YA MELI YA MV SPICE ISLANDERS, KATIKA HICHO WAMEKUBALIANA KUWEKA VITUO VYA DHARULA KATIKA MAENEO YA MKOANI,CHAKE NA WETE ILI KUPOKEA WATU WALIOPATWA NA MAAFA HAYO KWA KUWAPATIA HUDUMA.
 Baadhi ya abiria 525 waliookolewa kutoka katika Meli iliozama huko katika mkondo wa Nungwi Zanzibar wakiwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar
 Watoto waliookolewa kutoka ktika Meli iliozama ya Spici huko katika mkondo wa Nungwi zanzibar wakiwa katika Hospitali ya mnazi mmoja kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani.
 Umati wa watu wakiwa katika Hospitali ya mnazi mmoja kupata taarifa za watu wao kuhusiana na kuzama kwa meli ya Spice Islanders huko katika mkondo wa Nungwi
 Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni miongoni mwa Taasisi zilizokuwa mstari wa mbele katika harakati za uokoaji na usafirishaji wa maiti zilizopatikana kutoka katika meli iliozama ya spici iliokuwa ikielekea Pemba, kama wanavyoonekana katika picha.
  Mmoja kati ya waokozi akiwa katika hali ya majonzi baada ya kuchukuwammoja kati ya maiti zilizoletwa bandarini zanzibar na chombo cha bawe kutoka katika meli iliozama huko katika mkondo wa Nungwi.

 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akibadilishana mawazo na Naibu kadhi wa Zanzibar kutokana na msiba mkubwa uliotokea zanzibar jana.
 Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akizungumza na Madaktari huko katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar kuhusiana na Msiba mkubwa ulolikumba taifa letu la kuzama kwa meli ya Spici huko katika mkondo wa Nungwi kaskazini unguja.

Madaktari,Wauguzi na watu mbalimbali wakipokea maiti ya kwanza iliofikishwa huko katika viwanja vya  Maisara kutoka katika meli ya spici iliozama hapo jana huko katika mkondo wa Nungwi. PICHA ZOTE NA HAMAD HIJA-MAELEZO ZANZIBAR


MAMIA ya wananchi wakiwemo viongozi wakuu walimiminika katika viwanja vya Maisara na Hospital ya Mnazi mmoja pamoja na bandari kuu ya zanzibar ili kwenda kuona na watambuwa watoto wao wazee wao  ambao walikuwepo katika meli iliyopata ajali huko Nungwi ikielekea kisiwani Pemba hapo jana

Waliomiminika katika sehemu hizo kutoka sehemu mbali mbali za Unguja kunafuatia habari zilizoanza kutangazwa jana katika vyombo mbali mbali vya habari kwamba chombo cha Spice kimezama na ni kwamba kilikuwa kimechukuwa abiria kikielekea Pemba

Kwa mujibu wa habari zilizokuwa zikisimuliwa na baadhi ya wananchi waliofika hapo maisara wamesema kuwa suala kubwa lililochangia kutokea ajali hiyo ni kuwa vyombo vimechoka sana na wengine wamesema kuwa kujaa sana kwa chombo hicho hapo jana pia ni sababu ambazo zilichangia tukio hilo

Katika Viwaja vya Maisara umati wa watu ulikuwa umejaa kupita kiasi halikadhalika hata Hospital ya Mnazi mmoja umati ulikuwa umejaa vikle vile lengo kubwa la kuwepo hapo ni kuona na kuwatambua vijana wao ambao wameruhiwa na ambao wanapata matibabu

Halikadhalika umati mkubwa ulikuwa umejazana sana katika bandari mkuu ya Zanzibar ambapo maiti na majeruhi wa ajali hiyo walikuwa wakifikia hapo kutoka sehemu ya tokeo

Kufuatia ajali hii hiiitakuwa mara ya pili katika pindi cha nyuma meli yam v Fathi ilizama ambapo watu kadhaa wafariki dunia na baadhi ya mizigo ilpotea kutokana na ajali hiyo iliyotokea hapo nyuma

Kufuatia tokeo hilo wananchi wa zanzibar leo walikuwa wamejikusanya vikundi kila sehemu kuzungumzia tukio hili ambalo limetoke hapo jana likiwa limeacha majonzi makubwa kutokana na msiba huo uliotokea hapa zanzibar

AJALI YA MELI YA SPISE IRELAND HUKO NUNGWI KASKAZINI-UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa ni wenye huzuni sana wakati walifika eneo la tukio la ajali ya meli ya Spice Islander, iliyozama katika bahari ya Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi walionusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha jeshi la polisi (FFU) pamoja na wnaharakati wengine wa uokozi wakibeba majeruhi aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SpiceIslander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi Marium Mohamed Muradi (29) kutoka Tanga,aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SpiceIslander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. BALOZI SEIF ALI IDDI AKIONGOZWA NA NAIBU KADHI MKUU WA ZANZIBAR SHEKHE KHAMIS HAJI KHAMIS WAKITOKA NDANI YA HEMA MAALUM LILILOJENGWA KATIKA VIWANJA VYA MAISARA KWA AJILI YA KUPOKELEA MAITI ZA AJARI YA MV.SPICE ISLANDERS ILIYOKUWA IKITOKEA UNGUJA KWENDA PEMBA USIKU WA KUAMKIA LEO.
BALOZI SEIF ALI IDDI AKITOA MAELEKEZO JUU YA UTARATIWA WA KUFUATWA KWA WATU WATAKAOKUJA KUANGALIA MAITI ZAO NDANI YA HEMA, HADI MUDA HUU TAYARI MAITI MBILI ZIMESHA HIFADHIWA NDANI YA HEMA ILO TAYARI KWA KUTAMBULIWA KATIKA MAANDALIZI HAYO IDARA YA MAAFA WAKISHIRIKIANA NA OFISI YA MUFTI WA ZANZIBAR WATAZIHUDUMIA MAITI ZOTE KWA KUZIKOSHA,KUZIVIKA SANDA NA KUZIKA
WATU WALIOJAZANA KUANZIA UWANJA WA MAISARA HADI HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA WAKISUBIRI KUWATAMBUA MAITI ZAO,KARIBU MATAYARISHO YOTE YANAYO STAIKI KUFANYIWA MAITI YAMEKAMILIKA KINACHOSUBILIWA NI UPOKEAJI WA MAITI, TAYARI WATU WASIOPUNGUA 300 WAMEOKOLEWA WAKIWA WAZIMA WENGI WAO NI WATOTO NA KINAMAMA.