MSANII wa Bongo Flava, Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz aka Rais wa Wasafi hivi karibuni kafikishwa polisi kwa madai ya kushindwa kurudisha mkwanja aliokopa! Diamond alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam akidaiwa kujipatia mamilioni ya mkwanja za jamaa aitwaye Msafiri Peter aka Papaa Misifa,ambapo ilidaiwa kuwa Diamond alimuomba ampatie milioni 30 ili atoe albamu yake na wakaandikishiana mkataba kuwa atakuwa akimpa asilimia flani kiaina ya mauzo na mapato ya shoo atazokuwa anafanya.
Lakini Diamond amekuwa akienda kinyume mkataba huo na kwa sasa anadaiwa shilingi milioni 70, yaani milioni 30 alizochukua na milioni 40 za fidia ya kuvunja mkataba huo…. Papaa Misifa amekiri kumfikisha msanii huyo polisi na kumfungulia jalada la kesi lenye namba OB/RB/9343/11
Hivi sasa Diamond yuko nchini Sweden kupiga show
No comments:
Post a Comment