Tuesday, June 14, 2011

WANAFUNZI WA UDOM WAGOMA,60,WASIMAMISHWA MASOMO,IR WOTE WARUDISHWA NYUMBANI

Mgomo huu unakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya ule wa COLLAGE OF INFORMATICS AND VIRTUAL EDUCATION KATIKA CHUO KIKUU CHA UDOM.Ni mgomo ambao unashirikisha collage tatu ambazo ni SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES,EDUCATION NA  COLLAGE OF MINING

 Baadhi ya wanafunzi wa kitivo cha sayansi ya jamii wakiwa katika makundi makundi wakijadili suala la mafunzo kwa vitendo mara baada ya kubandikiwa tangazo ambalo linasema kuwa Hakuna mafunzo Kwa Vitendo
Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha wakisoma tangazo lililoandika kuwa hakuna mafunzo kwa vitendo lililobandikwa huku wengine wakijadili kiunagaunaga.
 Wanafunzi Wakimsikiliza kwa makini raisi wa kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na lugha Mh Mwakibinga Philipo Wakati akitoa Ufafanunuzi Na jinsi Serikali ya wanafunzi itakavyofanya kuhusiana na tatizo hilo
Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Akitoa maelezo kuhusiana na tangazo hilo linalosema kuwa hakuna field

Mnamo tarehe 20 disemba mwaka 2010 Wanafunzi Wa Kitivo cha Sayaynsi ya jamii sanaa na Lugha Waligoma kuingia madarasani Kwaajili ya kushinikiza kupewa mafunzo ya vitendo ambayo ni haki ya kila mwanafunzi wa elimu ya juu hali iliyopelekewa kutokea kwa ghasi aambazo polisi wa kutuliza ghasia walitumia nguvu pamoja na mabomu ya machozi ili kutuliza hali iliyochafuka kipindi hiko.

Mgomo huo ulidumu kwa suku mbili mfululizo hadi kupelekea Waziri Wa Elimu Shukuru Kawambwa na Mwenyekiti Wa Bodi Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma na Waziri Wa Mambo Ya Ndani Wa Nchi Mh Shamsi Vuai Nahodha Kufika Chuo Hapo Siku Ya Tatu na kuahidi Kulitafutia ufumbuzi na Kuwahidi wanafunzi hao kuwa watakwenda kufanya mafunzo kwa vitendo na kuuagiza Uongozi wa chuo Kuwatafutia Wanafunzi sehemu ya Kufanyia Mafunzo Kwa Vitendo.

Mara Baada ya Muda Kupita Chuo Kilianza Mpango Mzima Wa KUwatafutia Wanafunzi Sehemu Za Kufania Mafunzo Kwa Vitendo Na Kwa Kiasi kikubwa Wanafunzi Wengi waliweza Kupata nafasi hizo kwaajili ya kufanya mafunzo kwa vitendo katika kipindi Cha likizo huku wanafunzi wakionyesha wasiwasi wasiwasi wa kupata fedha zao za mafunzo kwa vitendo kitu ambacho Raisi Wa Kitivo Mh Mwakibinga Akasisitiza Kuwa Hawataingia Katika Mitihani ya Muhula Wa Mwisho bila Fedha kuingia katika akaunti zao kitu ambacho raisi wa kitivo hiko aliweza kukifuatilia na kuonyesha dalili za kuzaa matunda.

Hatimaye leo Majira ya Saa Saba Mchana katika viunga tofauti tofauti katika kitivo hiki walipigwa na mbumbuwazi mara baada ya kuonekana kwa tangazo ambalo linasema hakuna field huku Wazir wa Elimu Mh Kawambwa Aliahidi na Kusema kuwa Wanafunzi Wote Watakwenda Kufanya mafunzo kwa vitendo kitu ambacho kimezua maswali mengi hapa chuo, Wanafunzi wengi wamekuwa wakihoji kuhusu tangazo hilo ambalo linaonyesha kuwa na nembo ya chuo ambayo hutumika kwa matumizi ya kiofisi huku likikosa muhuli wa ofisi na hata saini ya mtoaji wa taarifa hizo wanafunzi hao walikaririwa wakisema kuwa hilo sio tangazo sahihi kwa sababu halina muhuli wa saini ya mtoaji, wakati  wakibishana Kuhusu uahalali wa muhuli kuwepo wengine wamesema kuwa hilo tangazo limetolewa na uongozi wa chuo kwa sababu aliyekuwa akibandika matangazo hayo aliletwa na gari la chuo kwa maana hiyo chuo kimemuagiza kufanya hivyo

Tatizo likaanzia hapa wanafunzi kuanza kudai viongozi wa serikali ya wanafunzi wawepo ili kutolea ufafanunuzi kitu ambacho Raisi wa KItivo Cha Sayansi Ya Jamii pamoja na Uongozi wake wote Wamewaambia Wanafunzi Wasubiri hadi kesho saa Tano Asubuhi ndio atatoa Majibu kama ni kweli Tangazo hilo limetolewa na Uongozi Wa Chuo Au Laaaahhhh.Hali ambayo inapelekea Wanafunzi Kuweza Kugoma Kwa sababu walishaahidiwa na wengine majina yao kutoka na kujua sehemu ya kufanyia mafunzo kwa vitendo leo hii unasema haluna mafunzo kwa vitendo wakati huo imebaki wiki moja kabla ya kuanza kufanya mitihani ya kumaliza muhula wa pili wa masomo

No comments:

Post a Comment