Saturday, June 11, 2011

WEMA SEPETU AHUKUMIWA MIAKA SITA JELA!

Muigizaji maarufu katika tasnia ya filamu hapa nchini na aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania, jana amehukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa Faini ya shilingi elfu 40 katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kumtukana matusi ya nguoni sanjari na kumtishia maisha msanii wa muziki wa kizazi kipya Bob Junior.

Hukumu ya kesi ilifunguliwa na Raheem Rummy Nanji "Bob Junior" Bob Junior alifungua kesi katika mahakama ya Mwanzo Kinondoni jijini Dar es Salaam, akimlalamikia Wema kumtukana matusi ya nguoni sanjari na kumtishia maisha. Kesi hiyo ambayo Wema alikiri kutenda kosa, Bob Junior alitakiwa kwenda na mashahidi tarehe 9 june.

Kabla ya kesi hiyo kutinga kwenye mahakama hiyo, Bob Junior alipeleka mashitaka yake kwenye kituo cha Polisi cha Osterbay, jijini Dar es Salaam na kufungua jalada la kesi namba OB/RB/6337/2011 MADAI: Kutishia maisha.

Wema hata hivyo hivi karibuni alisikika kwenye chombo kimoja cha Habari akiwaomba watanzania wamuombee kufuatia kesi hiyo. Aidha, alisema amebadilika na kuwa mwananchi mwenye maadili huku akilalamikia maisha yake ya nyuma kuwa yalichangia kumfikisha alipo sasa.

No comments:

Post a Comment