Tuesday, February 7, 2012

MILOVAN AWAKATAA NYOTA WAPYA SIMBA


LICHA ya uongozi wa Simba kuwaleta nyota watatu wa kimataifa kwa ajili ya kufanya majaribio kabla ya kuwapa mikataba, kocha mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic, amesema hana habari na wachezaji hao.

Simba imewaleta Nkanu Khumalo, Freddy Kamere kutoka Motema Pembe na AS Nika za DR Congo, pamoja na nyota mmoja aliyejulikana kwa jina la Kanu aliyekuwa akiichezea Cosmos ya Afrika Kusini, kwa lengo la kuwatumia katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kama itafanikiwa kutinga hatua hiyo.

Wachezaji hao wametua nchini Ijumaa iliyopita na walitarajiwa kuanza majaribio chini ya Cirkovic, lakini cha ajabu kocha huyo Mserbia amesema hajui chochote kuhusiana na ujio wa nyota hao.

Akizungumza na Mguso, Milovan alisema amewaona nyota hao mwishoni mwa wiki iliyopita lakini hajui lolote kuhusiana nao.

 “Hakuna ninachojua kiundani juu yao, lakini ukweli ni kwamba nimewaona wiki iliyopita lakini bado sijajua lolote, nadhani viongozi wa juu wanaweza kuliongelea hilo kwa kuwa hata leo (juzi) sijawaona mazoezini,” alisema Milovan na kuongeza:

“Binafsi bado sijapendekeza lolote kuhusu wachezaji ninaowataka kwa kuwa bado naendelea kuwafuatilia kwa karibu wachezaji waliopo sasa, lakini pengine niulize kwa kipindi kijacho naweza nikawa na majibu sahihi zaidi.”

No comments:

Post a Comment