LICHA ya kukosekana kwenye kikosi chake kwa takribani siku tano, Kocha Mkuu wa Yanga, Kosta Papic, amesema hatamweka benchi beki wake wa kati, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ .
Cannavaro aliondoka Yanga kwa siku tano na kuelekea kwao Zanzibar kwa ajili ya msiba wa dada yake kabla ya kurejea juzi Jumatatu.
Akizungumza na Mguso, Papic alisema licha ya kutokuwepo kambini, beki huyo lazima atacheza mechi ya leo dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“Licha ya Cannavaro kuchelewa kujiunga na wenzake kwenye mazoezi ya pamoja, hainifanyi nisimpange kwenye mechi ya Jumatano (leo). Ninaheshimu uwezo wake, sioni sababu ya kumweka benchi,” alisema Papic.
Cannavaro ndiye nguzo ya ulinzi kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment