Pamoja na kamati ya bunge ya Maendeleo ya jamii kukaa na madaktari waliogoma leo hii kwa lengo la kuzikutanisha pande mbili zinazovutana ili kufikia muafaka wa mgomo huo ambao umeingia siku ya 14 leo, imefahamika kwamba hali bado ni mbaya kutokana na kushindwa kufikia mwafaka kama ilivyotarajiwa.
Mwenyekiti wa madaktari Dr Steven Ulimboka amesema kwamba bado wanaendelea na mgomo kutokana na kutoridhishwa na serikali kutofanya kama wanavyotaka.
Dr Ulimboka amesema “mgogoro uko pale pale na hivi ninavyozungumza hospitali ya manispaa ya Temeke pia wameamua kusitisha kazi hali imekua mbaya zaidi pia toka mgogoro huu uanze huko Bugando Mwanza kwa sababu tatizo limekua kubwa sana, mimi kama kiongozi nasikitika sana na namna ambavyo serikali imekua inalichukulia hili swala”
Dr. huyoaliongeza zaidi kwamba “nawashangaa watendaji wa Wizara ya Afya ambao wamepotosha sana na ndio wanaohusika moja kwa moja kwenye mgogoro huu, wako wizarani na hatuoni wanachokifanya, ni wakati sasa wa kuwawajibisha”
kuhusu kikao walichofanya na kamati ya Bunge, Dr Ulimboka amesema “hatuwezi kuzungumzia Cotent ya majadiliano ni kitu ambacho kimakubaliano hatupaswi kukizungumza nje lakini kimsingi hakikua kikao cha maridhiano, ni kikao ambacho tulikwenda kuhojiwa ili ukweli ufahamike”
Bungeni Dodoma leo spika wa bunge Anne Makinda alizuia hoja ya kuahirisha shughuli za bunge na kujadili mgomo wa madaktari bingwa kuzungumziwa kwa kusema kwamba kazi hiyo wameshakabidhiwa kamati ya bunge ya maendeleo ya jamii.
No comments:
Post a Comment